UWEPO wa wachezaji nyota Lionel Messi na Cristiano Ronaldo umeshindwa kuwashawishi mashabiki kununua tiketi kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaozikutanisha Argentina na Ureno katika Uwanja wa Old Trafford. Muargentina Messi mwenye umri wa miaka 29 na Ronaldo kutoka Ureno na mchezaji wa zamani wa Manchester United mwenye umri wa miaka 29 wanatarajiwa kukutana katika mchezo huo lakini ni tiketi 15,000 pekee zilizokuwa zimeuzwa mpaka jana. Muandazi wa mechi hiyo Leo Morales amesema haelewi ni kwasababu gani tiketi zinauzika kwa kusuasua. Tiketi moja inauzwa kwa paundi 40 na Uwanja wa Old Trafford unaweza kubeba mashabiki 75,731.
No comments:
Post a Comment