MMOJA wa wadhamini wa klabu ya Sheffield United ametishia kujitoa kama klabu hiyo itamsajili tena Ched Evans ambaye alihukumiwa kwa kosa la kubaka. Tayari viongozi watatu wa klabu hiyo wameshajiuzulu toka ilipobainika jana kuwa evas mwenye umri wa miaka 25 anatkuwa akifanya mazoezi na timu yake hiyo ya zamani baada ya kutumikia adhabu yake ya kifungo jela. Ili kuweka sawa hali ya hewa meneja wa klabu hiyo Nigel Clough amesema hawajafikia uamuzi wowote mpaka sasa kama watamsajili au la. Katika taarifa yake kampuni ya inayojishughulisha na masuala ya ugavi ya DBL imedai kuwa wanapingana vikali na masuala ya ubakaji na vurugu hivyo watasitisha udhamini wao kama klabu hiyo ikiamua kumsajili tena Evans.
No comments:
Post a Comment