NGULI wa soka nchini Brazil Pele anaendelea vyema huku akitarajiwa kuruhusiwa kutoka hospitali leo baada ya kulazwa kutokana na maumivu ya tumbo. Nguli huyo mwenye umri wa miaka 74 alisitisha zoezi la kusaini vitabu katika makumbusho yaliyopewa jina lake huko Santos baada ya kulalamika maumivu ya tmbo jana. Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil na rafiki yake wa karibu Jose Fornos Rodrigues amesema Pele alifanyiwa vipimo na anaendelea vyema huku akitarajiwa kuruhusiwa leo. Pele ambaye aliisadia Brazil kushinda mataji matatu ya Kombe la Dunia, anahesabiwa kama mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika mchezo wa soka.
No comments:
Post a Comment