Thursday, November 13, 2014

SINA MPANGO KWA KUONDOKA MADRID - KHEDIRA.

KIUNGO wa klabu ya Real Madrid, Sami Khedira amesisitiza kuwa hajafanya mazungumzo na timu yeyote kufuatia tetesi ya klabu za Arsenal na Manchester United kumtaka. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani ana mkataba na mabingwa hao wa Ulaya ambao unamalizika kiangazi mwaka 2015 huku mazungumzo ya kuongeza mkataba yakiendelea. Klabu kadhaa zimekuwa zikifuatilia mwenendo wa mchezaji huyo huku United wakiwa tayari kumsajili katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani lakini Khedira mwenye umri wa miaka 27 amesisitiza kuwa ana furaha katika klabu yake ya sasa. Akihojiwa Khedira amesema hajawahi kufikiria kabisa kuondoka Madrid na hilo halibadilika bado kwani anaamini yuko katika timu bora hivyo hana sababu ya kumfanya aondoke.

No comments:

Post a Comment