KOCHA STUTTGART AJIUZULU KUFUATIA VIPIGO MFULULIZO.
MENEJA wa klabu ya VfB Stuttgart, Armin Veh amejiuzulu wadhifa wake huo leo, siku moja baada ya mabingwa hao wa zamani wa Bundesliga kuchapwa bao 1-0 na Augsburg na kubakia mkiano mwa msimamo wa ligi. Veh, ambaye aliingoza timu hiyo kushinda taji la Bundesliga mwaka 2007, amerejea msimu huu lakini baada ya kufungwa mechi tatu mfululizo ameamua kuachia ngazi. Katika taarifa yake Veh amesema ilikuwa ni hatua ngumu kuchukua kwasababu amekuwa karibu na timu hiyo lakini ana uhakika uamuzi wake ni sahihi. Stuttgart imefanikiwa kushinda mechi mbili msimu huu na kukubalia kufungwa mabao 26, wakiwa na safu mbaya ya ulinzi katika ligi sambamba na Werder Bremen wanaosika nafasi ya 17. Veh anakuwa kocha wa nne katika Bundesliga kubwaga manyanga msimu huu kufuatia Mirko Slomka wa Hamburg SV, Jens Keller wa Schalke na Robin Dutt wa Bremen nao kuachia ngazi.
No comments:
Post a Comment