MENEJA mpya wa klabu ya Inter Milan, Roberto Mancini amedai kuwa lengo lake kubwa ni kuirejesha timu hiyo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo wameshindwa kufuzu kwa kipindi cha miaka sita. Kauli hiyo ya Mancini imekuja kufuatia mpambano mkali na mahasimu wao AC Milan katika mchezo wa Serie A ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 jana. Mancini amesema wanahitaji muda lakini malengo yao ni kushinda mechi nyingi kadri iwezekanavyo ili waweze kumaliza katika nafasi tatu za juu katika msimamo wa ligi. Kocha huyo ambaye amewahi kuingoza Inter kushinda mataji saba yakiwemo matatu ya Serie kuanzia mwaka 2004 mpaka 2008, alipewa kwa mara nyingine mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya kutimuliwa kwa Walter Mazzarri wiki chache zilizopita. Katika kipindi chote ambacho Mancini alipokuwa akiinoa Inter amefanikiwa kushinda mara nne, kupoteza mara tano na sare moja katika michezo iliyowakutanisha na maahsimu wao wa jiji AC Milan.
No comments:
Post a Comment