MABINTI wa bondia nguli Muhammad Ali wamedai kuwa baba yao huwa anacheka akisikia tetesi za kuzushiwa kifo. Ali mwenye umri wa miaka 72 anaugua ugonjwa wa kutetemeka toka mwaka 1984 na kumekuwa na uvumi wa mara kwa mara kuwa afya yake imekuwa ikizorota. Lakini mabinti zake Maryum na Hana waliiambia BBC kuwa baba yao yuko katia hali njema na huwa anapenda kusikia watu wakimzungumzia kwani anaona kama vichekesho. Mabinti hao waliendelea kudai kuwa hata kama tetesi zinapotoka baba yao huwa na hamu kubwa kwani hufikiria kuwa atapamba kurasa za magazeti mbalimbali. Maryum amesema habari nyingi huwa zinatoka kwa watu ambao hawaufahamu vizuri ugonjwa hu ndio maana zinapotoshwa.
No comments:
Post a Comment