KLABU ya Real Madrid inakabiliwa balaa la majeruhi baada ya kiungo wake Luka Modric kutarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha mwaka huu baada ya kupata majeruhi wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa na timu yake ya taifa ya Croatia. Modric mwenye umri wa miaka 29 alianzishwa katika mchezo ambao Croatia walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Italia jana lakini alilazimika kutolewa baada ya dakika ya 28 ya mchezo kutokana na majeruhi. Kocha wa Croatia Niko Kovac alithibitisha kuumia kwa Modric na kudai kuwa wanasubiria vipimo zaidi kujua ukubwa wa tatizo lake. Modric amekuwa sehemu muhimu katika kikosi cha Madrid msimu huu akiwa amecheza katika mechi 17 za mashindano yote za timu hiyo. Kukosekana kwake kunaweza kutoa nafasi ya Sami Khedira kurejea katika kikosi cha kwanza kwa wiki chache zijazo baada ya Mjerumani huyo kushindwa kujihakikishia nafasi ya kuanza kutokana na majeruhi ya mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment