SHIRIKISHO la Soka la Nigeria-NFF limejiunga na waombolezaji wengine kufuatia kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa nchi hiyo, Yomi Peters. Peters alifariki dunia hospitalini jijini Lagos juzi akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kuugua saratani kwa kipindi kirefu. Katibu Mkuu wa NFF, Musa Ahmadu katika salamu zake za rambirambi amemuelezea Peters kama mmoja wa wanasoka aliyejituma zaidi enzi zake. Ahmadu amesema mashabiki wa soka ambao walimuona Peters enzi zake wakati aisakata kabumbu watakubaliana naye kuwa aliitumikia nchi yake kwa moyo wakati wote ambao alikuwa kivaa jezi za timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment