Wednesday, November 5, 2014

RONALDO AJINASIBU KUWA MCHEZAJI BORA WA WAKATI WOTE.

MCHEZAJI bora wa mwaka wa dunia, Cristiano Ronaldo anaamini atajumuishwa kama mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kucheza mchezo huo wakati utakapofikia wakati wake wa kustaafu. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alipokea tuzo yake ya kiatu cha dhahabu ikiwa ni mara ya tatu kwa kuwa mfungaji bora wa michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya jana huku pia akipewa nafasi ya kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya tatu Januari mwaka huu. Wakati akisisitiza kuwa bado ana miaka mingi ya kucheza soka katika kiwango cha juu, nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ana uhakika nafasi yake kama mmoja wa manguli wa soka katika historia tayari ameshajihakikishia. Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake hiyo Ronaldo amesema siku zote anataka kuwa bora ndio maana anafanya jitihada kila kukicha. Msimu huu Ronaldo bado ameendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga akiwa tayari ameshafunga mabao 22 katika mechi 16 za mashindano yote na kuiwezesha Madrid kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga sambamba na kutinga hatua ya timu 16 bora.

No comments:

Post a Comment