KIUNGO mahiri wa Manchester City, Yaya Toure amewaomba radhi mashabiki timu hiyo baada ya kupewa kadi nyekundu jana wakati wakipokea kipigo cha kushtusha kutoka kwa CSKA Moscow katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabao mawili yaliyofungwa na Seydou Doumbia yaliipa CSKA ushindi wao wa kwanza nchini Uingereza, wakati tukishuhudia Fernandinho akipewa kadi mbili za njano katika kipindi cha pili na Toure kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumsukuma Roman Eremenko. Matokeo hayo ynaifanya City ambao hawajashinda mechi hata moja kushika mkia katika kundi E na kuwaacha katika hatari ya kutolewa huku wakiwa wamebaki na mechi mbili dhidi ya Bayern Munich na AS Roma. Toure aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwaomba radhi mashabiki kwa kadi hiyo aliyopata pamoja na matokeo. Mbali na Toure Fernandinho naye aliomba radhi kwa kupata kadi ya pili ya njano ambayo ilisabababisha kikosi chao kuelemewa na kupoteza mchezo huo.
No comments:
Post a Comment