Wednesday, November 5, 2014

WACHEZAJI KUGOMEA KOMBE LA DUNIA LA QATAR KAMA LIKICHEZWA KIANGAZI - FIFPRO.

KIONGOZI wa Umoja wa Wachezaji wa Kulipwa unaojulikana kama Fifpro, amedai kuwa wachezaji wanaweza kugomea kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar kama itafanyika katika majira ya kiangazi. Joto katika nchi hiyo linaweza kufikia nyuzi joto 40 katika kipindi cha kati ya mwezi Mei na Septemba, ingawa muda haswa wa kufanyika michuano hiyo bado haujapangwa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA. Katibu mkuu Theo van Seggelen amesema Fifpro haitaweza kuruhusu wachezaji kuhatarisha afya zao. Van Seggelen aliendelea kudai kuwa kama ikibidi anaweza kulipeleka suala hilo mahakamani ili kupata haki ya msingi. Kiongozi huo amesema ana uhakika FIFA haitaweza kupingana na washauri wao wenyewe wa masuala ya afya kwa kuruhusu michuano hiyo kuchezwa majira ya kiangazi. Van Seggelen pia aliponda ombi la vilabu vya Ulaya kutaka michuano hiyo kufanyika katika kipindi cha Aprili na Mei akidai kuwa halina mashiko kwani bado kipindi hicho kinaweza kuhatarisha afya za wachezaji.

No comments:

Post a Comment