KLABU ya Tottenham Hotspurs imemruhusu Emmanuel Adebayor kurejea nyumbani kwao Togo kwa ajili ya sababu za binafsi. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester City amepewa muda wa kupumzika huku wakishindwa kufafanua zaidi. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa hawawezi kufafanua wa undani suala hilo kwani limekaa kibinafsi zaidi. Katika siku za karbuni Adebayor amekuwa katika mgogoro na familia yake akimtuhumu mama yake kumfanyia vitendo vya kichawi ili kuporomosha kiwango chake. Adebayor ameichezea Spurs mechi 12 msimu huu huku akiwa hajacheza toka Novemba wakati wa mapumziko kupisha mechi za kimataifa ambapo Togo ilishindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani.
No comments:
Post a Comment