Wednesday, December 10, 2014

RONALDO DI LIMA AMPIGIA CHEPUO WAJINA WAKE KUCHUKUA BALLON D'OR.

MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Brazil, Ronaldo Di Lima, amesema hana shaka kuwa Cristiano Ronaldo atanyakuwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ndio anapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo lakini anakabiliwa na changamoto kutoka kwa nyota wa Barcelona Lionel Messi na golikipa wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich Manuel Neuer. Pamoja na hayo, Ronaldo ambaye amewahi kushinda Kombe la Dunia mara mbili akiwa na Brazil amesema wajina wake huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye aliiongoza Real Madrid kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita ana nafasi ya wazi kushinda tuzo hiyo. Ronaldo amesema inafurahisha kuiona Madrid ikicheza kwani ni timu yenye wachezaji wenye ubora akiwemo Cristiano Ronaldo ambaye amekuwa akiongeza chachu katika kila mchezo anaocheza. Nguli huyo aliendelea kudai kuwa kwa mwaka huu hakuna mashaka yeyote kwamba Ballon d’Or itakuwa kwa ajili ya Ronaldo.
0000

No comments:

Post a Comment