Wednesday, December 17, 2014

AFUNGIWA MWAKA MMOJA KWA KUKATAA KUPOKEA MEDALI.

BONDIA wa ngumi za ridhaa Laishram Sarita Devi kutoka India amefungiwa mwaka mmoja baada ya kukataa kupokea medali yake ya shaba katika michuano ya bara la Asia iliyofanyika Korea Kusini Octoba mwaka huu. Sarita mwenye umri wa miaka 29 alionekana kutofurahishwa na matokeo ya kupigwa katika hatua ya nusu fainali na bondia Park Ji-na aliyekuwa akipewa nafasi ya kushinda hivyo kugoma kupokea medali hiyo. Bondia huyo ambaye mara ya kwanza alikuwa amefungiwa maisha sasa anatarajiwa kurejea tena ulingoni Octoba mwakani. Akizungumzia adhabu yake hiyo mpya Sarita aliondoka jukwaani wakati kabla ya kupokea medali yake amesema hiyo imekuwa ahueni kubwa. Hata hivyo, Chama cha Ngumi za Ridhaa cha India klimedai kuwa kitaiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la mchezo huo ili kuomba adhabu hiyo ipunguzwe zaidi.

No comments:

Post a Comment