Wednesday, December 17, 2014

RUFANI YA ALLEGRI YAKUBALIWA.

SHIRIKISHO la Soka la Italia limekubali rufani ya meneja wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri. Allegri alifungiwa mechi moja lakini sasa anaweza kuwepo katika benchi la ufundi la timu hiyo wakati Juventus itakapocheza na Cagliari baadae leo. Kocha huyo alilimwa adhabu hiyo baada ya kumshambulia mwamuzi wakati wa mchezo wa Serie A dhidi ya Samdoria. Badala ya kufungiwa mechi moja sasa kcha huyo atalazimika kulipa faini ya euro 10,000.

No comments:

Post a Comment