OFISA mkuu wa maadili aliyehusika katika uchunguzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Michael Garcia amejiuzulu wadhifa wake huo. Garcia aliongoza uchunguzi wa FIFA kuhusiana na madai ya ufisadi katika kutafuta wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022. Katika taarifa yake ya kujiuzulu Garcia amesema kuwa kuna ukosefu wa uongozi katika FIFA na kwamba alikuwa amepoteza imani na mwanachama mwenzake katika kamati hiyo ambaye ni jaji Joachim Eckert kutoka Ujerumani ambaye amedai hakusema ukweli kuhusu matokeo ya uchunguzi wake. Rais wa FIFA Sepp Blatter amesema ameshangazwa na uamuzi wa Garcia lakini kazi katika kamati hiyo ya maadili itaendelea kama kawaida pamoja na kutokuwepo kwake.
No comments:
Post a Comment