Wednesday, December 17, 2014

SIHUSIKI NA SUALA LA UPANGAJI MATOKEO - HERRERA.

KIUNGO wa klabu ya Manchester United, Ander Herrera amesisitiza kuwa hajawahi kushiriki zoezi lolote la upangaji matokeo wakati akiitumikia timu ya Real Zaragoza. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania ametajwa katika kundi la wachezaji wakiwemo pia makocha na wakurugenzi katika uchunguzi wa kashfa ya upangaji matokeo katika Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga. Herrera aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook kuwa hajawahi na kamwe hatathubutu kujihusisha na suala la upangaji matokeo kwani anaupenda mchezo wa soka na anaamini katika mchezo wa haki ndani na nje ya uwanja. Waendesha mashitaka katika kashfa hiyo wanadai kuwa fedha taslimu euro 965,000 zililipwa kwa kocha Javier Aguirre na wachezaji tisa wa Zaragoza, ikiwa ni pamoja na Herrera, kabla ya mchezo wa La Liga mwishoni mwa msimu wa 2010-2011. Herrera aliondoka Zaragoza na kujiunga na timu ya nyumbani kwao ya Athletic Bilbao mwezi Agosti 2011, kabla ya kujiunga na United mwezi Juni 2014.

No comments:

Post a Comment