MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Arsenal, Thierry Henry ametangaza kustaafu soka rasmi leo. Nyota huyo aliyetwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 akiwa na Ufaransa alijiondoa kwenye klabu yake ya New York Red Bulls ya marekani mapema mwezi huu na kukawa na tetesi atachagua kujiunga na klabu nyingine kubwa barani Ulaya. Lakini badala yake alitangaza kutundika dariga zake na kuwashukuru mashabiki wake, wachezaji wenzake aliocheza nao katika vilabu mbalimbali na watu binafsi kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichokuwa akisakata kabumbu. Henry alianza kuibuka katika klabu ya Monaco kabla ya Juventus kumuona na kumsajili na baadae kutimkia Arsenal ambako aliitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na kwenda Barcelona na baadae New York Red Bulls.
No comments:
Post a Comment