WAZIRI wa habari nchini Algeria Mohammed Tahmi amesisitiza kwamba kifo cha mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Albert Ebosse kilisababishwa na mashabiki waliokuwa wakirusha vitu. Tahmi ambaye alikuwa akizungumza na radio ya Algeria alikuwa akijibu ripoti ya wiki jana ya daktari wa kuchunguza mauaji kwamba majereha ya Ebosse yalisababishwa na mashambulizi. Ebosse mwenye umri wa miaka 25 aliaga dunia Agosti 23 mwaka huu baada ya klabu yake JS Kabylie kupoteza mchezo nyumbani. Tahmi amesema walifanya uchunguzi wao ambao ulionyesha kuwa mchezaji huo aliuawa kutokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali kutoka kwa mashabiki waliogadhabishwa na timu yao kufungwa. Waziri huyo aliendelea kudai kuwa vitu vilirushwa kutoka pande zote mbili na wachezaji wote walilengwa wakati wakielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo lakini kwa bahati mbaya tukio likamtokea Ebosse. Suala hilo kwa sasa liko mahakamani ambapo uamuzi utatolewa.
No comments:
Post a Comment