Friday, December 12, 2014

ALGERIA ITASHINDA TAJI LA AFCON - NASRI.

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri amedokeza kuipigia chapuo Algeria kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta mapema mwakani. Nasri mwenye umri wa miaka 27 ambaye amezaliwa jijini Marseille amesema naiunga mkono Algeria nchi ambayo ndio asili ya wazazi wake na amekuwa akitizama mechi zao maa kwa mara. Nyota huyo anayecheza Manchester City amesema alifurahi kuona Algeria wakifanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil ambako walitolewa katika hatua ya mtoano jambo ambalo liliwashangaza wengi. Nasri alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotuma salamu za kupongezi kwa Algeria wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwingine akiwa Frank Ribery ambaye mke wake ni raia wan chi hiyo. Algeria imepangwa katika kundi C sambamba na timu za Senegal, Ghana na Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment