MENEJA wa klabu ya Newcastle United, Alan Pardew ametajwa kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu huku mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero yeye akipewa tuzo hiyo kwa upande wa wachezaji. Pardew mwenye umri wa miaka 53 ameingoza Newcastle kushinda mechi tatu kati ya nne na kunyakuwa tuzo hiyo mbele ya meneja wa Chelsea Jose Mourinho na Manuel Pellegrini wa City. Washambuliaji wa Queens Park Rangers, Charlie Austin, Danny Ings wa Burnley na Aguero wote wamefunga mabao matatu kila mmoja mwezi uliopita lakini tuzo amekwenda kwa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina. Hiyo inakuwa mra ya pili kwa Aguero kushinda tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment