Friday, December 12, 2014

BUTTON BADO ATAMANI KUENDELEA KUBAKIA MCLAREN.

DEREVA mahiri wa magari ya langalanga, Jenson Button amesema ana matumaini ya kubakia katika timu ya McLaren zaidi ya mwaka 2015. Dereva huyo mwingereza alitangazwa kupewa mkataba mpya wa McLaren jana ambapo sasa atakuwa akiendesha sambamba na Fernando Alonso katika timu hiyo. Button amepewa mkataba wa miaka miwili huku akiahidiwa kuongezewa kama atakuwa katika kiwango kizuri. Akihojiwa Button amesema kuendelea kuwepo katika timu hiyo ni jambo muhimu na atajitahidi kadri awezavyo kuhakikisha anashinda taji la dunia.

No comments:

Post a Comment