WAJENZI katika mji wa Mongomo wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanamaliza ujenzi katika moja ya viwanja vine ambavyo vitatumika kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani huku wakiwa wamebakiwa na mwez mmoja. Mongomo mji ambao ni nyumbani kwa rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang, sambamba na Ebebeyin, Bata na Malabo ndio iliyopangwa kuwa miji wenyeji wa michuano hiyo. Guinea ya Ikweta ilikubali kuandaa michuano hiyo mwezi uliopita ikiitikia mwito wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF baada ya Morocco kujitoa kutokana na hofu ya maambukizi ya Ebola. Viwanja vilivyopo Malabo na Bata vyote vilitumika katika michuano hiyo wakati nchi hiyo ilipoandaa kwa pamoja na Gabon mwaka 2012. Hata hivyo viwanja vilivyopo katika miji ya Ebbeyin na Mongomo vyote vinahitaji matengenezo ili kufikia ubora wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment