MUNTARI AANZA MAZOEZI.
KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Ghana, Sulley Muntari anakaribia kupona kabisa baada ya kuonyesha dalili njema mazoezini. Nyota huyo wa AC Milan alipata majeruhi ya nyonga ambayo yalimfanya kukaa nje kwa siku kadhaa lakini amekuwa akishiriki mazoezi kwa siku mbili hivyo kuonyesha dalili njema. Muntari amekosa mechi dhidi ya Udinese na Genoa lakini meneja wa Mila Filipo Inzaghi sasa anaweza kumtumia katika mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Napoli. Taarifa hiyo imekuja katika wiki ambayo kumekuwa na ripoti kutoka Ghana zinazodai kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo ana mpango wa kuwarejesha wachezaji wote wenye utata katika kikosi chake. Alhamisi iliyopita Grant alikaririwa akidai kuwa yuko tayari kumpokea mchezaji yeyote ambaye atakuwa tayari kujitolea kwa kila kitu kwa ajili ya nchi yake. Ghana inatarajiwa kuanza rasmi maandalizi yake ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani katika wiki mbili zinazokuja.
No comments:
Post a Comment