MENEJA wa klabu ya AC Milan, Filippo Inzaghi amedai kuwa hawezi kumaliza kumaliza matatizo yote yanayoikabili timu hiyo kwa mara moja. Milan wameshinda mara moja kati ya mechi saba za Serie A walizocheza hivyo kuwafanya kuwa nyuma kwa alama tano kufikia nafasi tatu za juu katika msimamo wa ligi. Inzaghi ambaye alichukua mikoba ya Clarence Seedorf kiangazi mwaka huu, ana uhakika wa kurejesha makali katika timu hiyo lakini anahitaji muda, uvumilivu na uelewa ili waweze kufikia huko. Kocha huyo amesema hana maajabu yeyote kusema kwamba anaweza kuondoa matatizo yote yaliyopo Milan lakini kama kutakuwa na utulivu na uvumilivu ni wazi kuwa watafikia malengo waliyojiwekea. Inzaghi amesema kwasasa sio Milan pekee wanaosuasua kwani ukiwaangalia mahasimu wao Inter Milan na Napoli wote wana matatizo ya hapa na pale. Msimu uliopita Milan walimaliza nje ya timu sita bora kwa mara ya kwanza toka msimu wa mwaka 1997-1998.
No comments:
Post a Comment