KIUNGO wa zamani wa klabu ya Arsenal, Gilberto Silva amebainisha kuwa aliitwa na timu hiyo ili apewe nafasi katika benchi la ufundi. Mbrazil huyo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal ambacho kilimaliza msimu wa mwaka 2003-2004 bila kufungwa katika Ligi Kuu, amepania kuwa kocha siku za usoni. Akihojiwa Silva aalikiri kupata mualiko huo na kudai kuwa kila kitu kinawezekana huku akifurahia kupata mialiko kama hilo. Silva aliendelea kudai kuwa suala hilo linamfurahisha na kumuongezea nguvu kwani anapenda kujifunza kwa wengine na kupata uzoefu wa kutosha ambao utamfanya kuimarika kwa staili yake wake mwenyewe. Hata hivyo nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 amesema bado kwasasa anataka kuendelea kusakata kabumbu.
No comments:
Post a Comment