Monday, December 22, 2014

MANCINI ACHOMOA TAARIFA ZA KUMTAKA LENNON.

MENEJA wa klabu ya Inter Milan, Roberto Mancini amepuuzia taarifa kuwa anajaribu kumsajili winga wa klabu ya Tottenham Hotspurs Aaron Lennon ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kikosi chake kuelekea mzunguko wa pili wa msimu. Taarifa hizo zilidai kuwa Lennon ambaye ameshindwa kupata namba katika kikosi cha cha kwanza cha Spurs, atakuwa mmoja ya wachezaji watakaowindwa na Mancini katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Lakini baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Lazio jana, Mancini amedai kuwa Lennon hayuko katika mipango yake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wakati utakapofika ataweka bayana mipango yake ya kuimarisha kikosi lakini kwasasa hizo habari zilizotoka sio kweli. Inter kwasasa inashika nafasi ya 11 katika Serie A wakitofautiana alama 18 na vinara Juventus.

No comments:

Post a Comment