Monday, December 22, 2014

NAPOLI ITAENDELEA HATA BILA YA BENITEZ - LAURENTIIS.

RAIS wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amesisitiza kuwa mipango ya timu hiyo itaendelea kama ilivyopangwa hata kama Rafa Benitez hatakuwepo. Mustakabali wa kocha huyo raia wa Hispania umekuwa mashakani kutokana na matokeo yasiyo ya kuridhisha ambayo yamepelekea timu hiyo kuenguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa. Akihojiwa rais huyo amesema anadhani tayari Napoli ni timu imara Italia na Ulaya lakini itahitaji subiora kwani kwasasa hawawezi kuwa na viungo wawili wanaolipwa kati ya euro milioni 8 hadi 10 kwa mwaka. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kama Benitez hatakuwa na uvumilivu na kusubiri basi wanaweza kuendelea na mipango yao bila uwepo wake.

No comments:

Post a Comment