Tuesday, December 16, 2014

ROAD TO AFCON: YAHIA AOMBA KUACHWA NA TUNISIA.

BEKI wa kimataifa wa Tunisia, Alaedinne Yahia ameomba kutoitwa katika timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika mapema mwakani. Beki huyo wa kati mwenye uzoefu mzaliwa wa Ufaransa, ameichezea Tunisia mechi 22 na alikuwa sehemu ya kikosi cha nchi hiyo kilichonyakuwa taji la michuano hiyo mwaka 2004. Yahia alimtaarifu kocha wan chi hiyo Mbeligiji Georges Leekens kuwa hayuko tayari kuitumikia katika michuano hiyo itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta. Yahia mwenye umri wa miaka 33, amesaini mkataba mpya na klabu ya Caen ya Ufaransa Octoba mwaka huu na ameamua kuhamishia nguvu zake katika kuisaidia timu yake baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu kutokana na majeruhi ya goti. Leekens amesema anaheshimu uamuzi wa Yahia wa kutotaka kuitwa katika timu ya taifa kwasababu anajiona hayuko fiti kiafya na kiakili kwa ajili ya michuano hiyo. Katika michuano hiyo Tunisia imepangwa katika kundi B sambamba na timu za Cape Verde, Zambia na DR Congo.

No comments:

Post a Comment