MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemaliza mwaka kwa staili ya aina yake kwa kubeba tuzo ya mchezaji bora wa mwaka au Globe Soccer Awards huko Dubai. Ronaldo amekuwa na mwaka mzuri huku akivunja rekodi kwa kuwa na mabao mengi katika msimu mmoja wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati alipoiongoza Real Madrid kunyakuw ataji lake la 10 la michuano hiyo. Nyota huyo pia anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa mara ya pili mfululizo Januari 12 mwakani lakini anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Lionel Messi na Manuel Neuer. Ronaldo ambaye alikuwepo mwenyewe kupokea tuzo hiyo katika sherehe zilizofanyika katika Hotel ya Atlantis Palm aliwashukuru mashabiki, wachezaji wenzake na viongozi wa Real Madrid kwa ushirikiano wanaompa na kufanya kupata mafanikio hayo. Kwa upande mwingine kocha wa Madrid Carlo Ancelotti naye alitunukiwa tuzo hiyo kama kocha wa bora wa mwaka kutokana na mafanikio aliyoipa timu hiyo kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment