MMILIKI wa klabu ya Birmingham David Sullivan amedai timu hiyo ingeweza kumsajili Cristiano Ronaldo kwa paundi milioni sita kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2003. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alisajiliwa na United iliyokuwa chini ya Sir Alex Ferguson akiwa na umri wa miaka 18 akitokea klabu ya Sporting Lisbon kwa kitita cha euro milioni 15.5. Ronaldo aliitumikia United kwa miaka sita akishinda taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na matatu ya Ligi Kuu kabla ya kusajiliwa na Real Madrid mwaka 2009. Hata hivyo, Sullivan amedai kuwa Birmingham ingeweza kumnasa kinda huyo ambaye aliletwa kwao kabla ya kuchagua kujiunga na United. Sullivan amesema kabla ya Ronaldo kwenda United walimpa ofa ya paundi milioni sita lakini baadae alichagua kwenda Old Trafford badala yao.
No comments:
Post a Comment