SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limesema litaupitia upya utaratibu wa kumpata mshindi kwa njia ya bahati nasibu baada ya timu kuwa sawa katika hatua ya makundi. Hatua hiyo inakuja kufuatia jana Guinea kutinga robo fainali kwa ushindi wa mezani baada ya kubahatika kwenye bahati nasibu hiyo huku Mali ikifungasha virago baada ya timu zote mbili kumaliza mechi za makundi zikiwa zote zina alama tatu sawa na mabao matatu ya kufunga. Katika mechi za kundi D zilizomalizika juzi ni Ivory Coast pekee ndio waliokuwa wamesonga mbele baada ya kuifunga Cameroon kwa bao 1-0. Wadau wengi na mashabiki wa soka wameukosoa utaratibu huo wa bahati nasibu wakidai kuwa hautendi haki. Mkurugenzi wa habari wa CAF Junior Binyam amesema pamoja na kwamba walipaswa kusimamia kanuni za mashindano hayo lakini anadhani ipo haja ya kuboresha utaratibu wa kumpata mshindi pindi tukio kama hilo linapotokea. Binyam aliendelea kudai kuwa sio haki kwa timu kurudi nyumbani kama ilivyofanyika kwa Mali.
No comments:
Post a Comment