KLABU ya Arsenal imethibitisha kumsajili kiungo chipukizi Krystian Bielik kutoka klabu ya Legia Warsawa ya Ukraine kwa kitita cha paundi milioni 2.4. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye alifanyiwa vipimo vya afya wiki iliyopita alisajiliwa na Legia akitokea klabu ya Lech Poznan ya Poland Julai mwaka jana akiwa amecheza mechi sita katika mshindano yote msimu huu. Bielik ambaye amewahi kukichezea kikosi cha timu ya taifa ya Poland kwa vijana chini ya umri wa miaka 16, ana uwezo wa kucheza nafasi zote kama kiungo mkabaji au nafasi ya beki wa kati. Kuna taarifa kuwa Bielik anaweza kuingizwa katika kikosi cha kwanza cha Arsenal moja kwa moja kutokana na uwezo mkubwa alionao.
No comments:
Post a Comment