KATIKA habari za tetesi za usajili barani Ulaya ni pamoja na klabu ya Manchester United imemthaminisha kwa paundi milioni 50 golikipa wake David de Gea mwenye umri wa miaka 24 ambaye anawindwa na Real Madrid. Beki wa kimataifa wa Ujerumani Mats Hummels mwenye umri wa miaka 26 amezinyong’onyesha klabu za Manchester United, Liverpool na Chelsea kwa kudai kuwa anataka kuendelea kubakia Borussia Dortmund. Nyota wa kimataifa wa New Zealand na klabu ya West Ham United Winston Reid mwenye umri wa miaka 26 ameipasha klabu hiyo kuwa hatasaini mkataba mpya kwani anataka kujiunga na Arsenal. Klabu ya Wolfburg ya Ujerumani iko tayari kutoa kitita cha paundi milioni 23 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Andre Schurrle mwenye umri wa miaka 24 lakini Chelsea wenyewe wanataka paundi milioni 30. Kiungo wa Arsenal Francis Coquelin mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kupewa mkataba mpya na klabu hiyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa toka arejeshwe kutoka Charlton Athletic alipokwenda kwa mkopo. Naye kiungo wa Manchester United Darren Fletcher mwenye umri wa miaka 30, anahusishwa na taarifa za kwenda Valencia kutokana na kushindwa kupata namba katika kikosi cha Louis van Gaal lakini anaweza kuamua kubakia Ligi Kuu kutokana an kutakiwa na klabu ya West Ham United.

No comments:
Post a Comment