BILIONEA Wang Jianlin kutoka China amenunua hisa ya asilimia 20 katika klabu ya Atletico Madrid kwa kiasi cha paundi milioni 34 huku akijipanga kuongeza zaidi hisa zake katika siku za usoni. Bilionea huyo ambaye anamiliki kampuni kubwa ya Dalian Wanda anatajwa kama mmoja matajiri wakubwa wa China akiwa nyuma ya bilionea wa Alibaba Jack Ma. Kampuni hiyo itakuwa ya kwanza kutoka China kuwekeza katika klabu kubwa barani Ulaya. Wang amesema uwezkezaji huo utatoa nafasi kwa wachezaji wanaochipukia kutoka China kupelekwa Ulaya na Wanda na kusajiliwa na vilabu vikubwa. Wang pia aliendelea kudai kuwa uwekezaji huo utaimariisha soka la nchi hiyo na kupunguza pengo lililokuwepo na mataifa mengine duniani. Mabilionea kadhaa kutoka Asia wamepata muamko wa kuwekeza katika vilabu mbalimbali barani Ulaya akiwemo bilionea kutoka Malaysia Vincent Tan anayemiliki klabu ya Cardiff City. Wengine ni bilionea anayemiliki shirika la ndege la AirAsia Tony Fernandez ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Queens park Rangers na bilionea wa Singapore Peter Lim ambaye anamiliki hisa katika klabu ya Valencia.
No comments:
Post a Comment