RAIS wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema klabu hiyo inafikiria kusitisha udhamini wa fulana zao na Qatar kwasababu ya wasiwasi wa mambo ya kijamii katika taifa hilo. Akizungumza katika mahojiano Bartomeu amesema kwasasa Barcelona inaangalia uwezekano wa kupata wadhamini wengine pindi mkataba wao na Qatar utakapomaliza mwakani. Bartomeu aliendelea kudai kuwa walisaini mkataba huo miaka minne iliyopita kutokana na sababu za kiuchumi na kuongeza hivi sasa kuna masuala ya kijamii yanapaswa kuangaliwa kabla ya kusaini mkataba mpya. Barcelona walitengeneza vichwa vya habari Desemba mwaka 2010 wakati walipomaliza mgomo wao kutovaa nembo yeyote ya mdhamini katika fulana zao kwa kusaini mkataba uliokuwa na thamani ya euro milioni 30 kwa mwaka na Qatar Foundation.
No comments:
Post a Comment