KLABU ya Manchester United imerejea tena katika orodha za juu za vilabu tajiri ambapo sasa wamepaa mpaka nafasi ya pili katika klabu zinazoingiza fedha nyingi wakiwa nyuma ya vinara ya Real Madrid. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo, mapato ya vilabu 20 tajiri vilivyomo katika orodha hiyo yamepanda mpaka kufikia euro bilioni 6.79 kwa msimu wa 2013-2014 ikiwa ni ongezeko la euro milioni 873 ukilinganisha na misimu ya nyuma. Mabingwa Ulaya Madrid wao wanaongoza orodha hiyo kwa miaka 10 mfululizo lakini Ligi Kuu Uingereza imeendelea kuonyesha kwamba wana nguvu za kiuchumi kwa nane kutoka huko kuingia katika orodha hiyo. Pamoja na msimu mbovu waliokuwa nao msimu uliopita United bado imepaa kwa nafasi mbili na kuwa klabu ya pili duniani inayoingiza fedha nyingi zaidi duniani kutokana na mapato ya euro milioni 565. Klabu za Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool zote zimechomoza katika orodha ya 10 bora wakati Tottenham Hotspurs wao wapo katika nafasi ya 20 bora sambamba na Newcastle United na Everton wanaongia katika orodha hiyo kwa mara ya kwanza. Barcelona waliokuwa wakishika nafasi ya pili safari hii wameanguka mpaka nafasi ya nne kwa kuingiza mapato ya euro milioni 528 huku mabingwa Bayern Munich wao wakiwa nafasi ya tatu kwa kuingiza euro milioni milioni 531. Paris Saint-Germain wako katika nafasi ya tano wakiingiza kiasi cha milioni 517 wakifuatiwa na Manchester City katika nafasi ya sita wakiliongiza euro milioni 452, nafasi ya ssaba inakwenda kwa Chelsea waliongiza euro milioni 423. Wengine ni Arsenal katika nafasi ya nane waliongiza euro milioni 412.3 wakifuatiwa na Liverpool katika nafasi ya tisa waliongiza kiasi cha euro milioni 334 na Juventus ndio wanaofunga orodha ya 10 bora kwa kuingiza euro milioni 279.4. Kwa upande wa timu nyingine za Uingereza zilizopo katika orodha ya 20 bora, Spurs wao wako katika nafasi ya 12 kwa kuingiza kiasi cha euro milioni 104.9 wakati Newcastle waliongiza euro milioni 169.4 na Everton euro milioni 157.3 wako katika nafasi ya 19 na 20.
No comments:
Post a Comment