WINGA mahiri wa kimataifa wa Uingereza Theo Walcott amedai kuwa safu ya sasa ya ushambuliaji ya Arsenal ni bora kuliko ile ya mwaka 2006. Walcott alijiunga na Arsenal mwaka huo na kucheza sambamba na baadhi ya wachezaji waliokuwepo katika kikosi ambacho kilimaliza msimu bila kufungwa mwaka 2003-2004 akiwemo Thierry Henry na Dennis Bergkamp. Lakini Walcott ambaye alitokea Southampton kabla ya kujiunga na Arsenal amesema safu ya ushambuliaji ya sasa yenye kuwajumuisha Alexis Sanchez, Olivier Giroud, Danny Welbeck na Alex Axlade-Chamberlain ndio imara zaidi. Walcott amesema kikosi cha sasa ndio bora ila wanatakiwa kuthibitisha ubora wao kwa matokeo watakayopata.
No comments:
Post a Comment