BAADA ya vigogo wa soka wa Afrika Ivory Coast kutinga fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika jana, leo kuna mchezo mwingine utakaowakunanisha wenyeji Guinea ya Ikweta na Ghana. Timu hizo zitajitupa katika Uwanja wa Bata usiku huu kutafuta nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo. Katika nusu fainali iliyochezwa jana Ivory Coast waliizidi maarifa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC na kuitandika bila huruma mabao 3-1. Mabao ya Ivory Coast yalifungwa na Yaya Toure katika dakika ya 20, Gervinho dakika ya 41 na Wilfried Kanon dakika ya 68 huku lile la kufutia machozi la DRC lilifugwa kwa penati na Mbokani Bezua katika dakika ya 24. Mchezo wa fainali ya michuano ya hiyo unatarajiwa kuchezwa Jumapili hii.
No comments:
Post a Comment