DIRISHA dogo la usajili nchini Uingereza limefungwa jana usiku huku Chelsea ikiwa ndiyo timu inayoongoza kwa kutumia fungu katika usajili kwa kumchukua winga wa kimataifa wa Colombia Juan Cuadrado kwa kitita cha paundi milioni 23.3. Kwa ujumla klabu za Ligi Kuu zimetumia kiasi cha paundi milioni 130 katika usajili huu hivyo kufikia kiwango kama walichotumia mwaka jana. Klabu ya Crystal Palace ndio iliyokuwa na harakati nyingi katika siku ya mwisho ya usajili kwa kuwachukua wachezaji wanne akiwemo Wilfried Zaha. Klabu ya Hull City ndio iliyofunga dirisha hilo kwa kutangaza usajili wa kumchukua mshambuliaji wa Lokomotiv Moscow Dame N’Doye katika muda wa mwisho. Jumla ya wachezaji 13 wamesajiliwa katika siku ya mwisho ya usajili huku 35 zaidi wakisajiliwa katika kipindi chote toka dirisha lilipofunguliwa Januari mosi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment