KOCHA wa zamani wa klabu za Bayern Munich na Barcelona Udo Lattek amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80. Kocha huyo raia wa Ujerumani alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kutetemeka au Parkinson kama yale yanayomsumbua nguli wa masumbwi wa Marekani Mohamad Ali. Lattek atakuambukwa kwa vipindi viwili alivyoingoza Bayern na kuiwezesha klabu hiyo kunyakuwa taji lake la kwanza la Ulaya mwaka 1974. Kocha huyo pia alikuwepo katika benchi la ufundi la kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani Magharibi katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1966 ambapo walichapwa na Uingereza katika Uwanja wa Wembley.
No comments:
Post a Comment