Thursday, February 5, 2015

ANCELOTTI ATHIBITISHA KUWAKOSA RODRIGUEZ NA RAMOS KATIKA MCHEZO DHIDI YA MAHASIMU WAO ATLETICO JUMAMOSI HII.


MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa James Rodriguez na Sergio Ramos watakosa mchezo wa La Liga dhidi ya mahasimu wao jiji Atletico Madrid Jumamosi hii. Wawili hao walipata majeruhi katika mchezo wa jana ambao waliitandika Sevilla kwa mabao 2-1, ambapo Ramos alipata majeruhi ya msuli wa paja huku Rodriguez yeye akipata majeruhi katika mguu wake wa kulia baada ya kufunga bao la kuongoza. Ancelotti sasa anakabiliwa na uhaba wa mabeki kutokana na beki wake wa kati Pepe naye kuwa nje kutokana na majeruhi ya mbavu. Hata hivyo, Ancelotti ana matumaini chipukizi Raphael Varane na Nacho wataweza kumudu changamoto za Atletico iliyo chini Diego Simeone. Akihojiwa Ancelotti amesema pamoja na kuwakosa mabeki wake kutegemea lakini bado ana imani na waliopo akiwemo Nacho na Varane kwamba wataweza kuhimilia mikikimikiki ya wapinzano wao hao Jumamosi.

No comments:

Post a Comment