Thursday, February 5, 2015

BARCELONA NAO MBIONI KUBADILI JINA CAMP NOU.

OFISA mkuu wa Shirika la Ndege la Qatar, Akbar Al Baker amebainisha kuwa jina la kampuni hiyo linaweza kuongezwa Camp Nou kufuatia majadiliano na Barcelona kuhusiana na mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa kampuni hiyo wakiwa kama wadhamini wakuu unatarajiwa kumalizika mwaka 2016 na wako tayari kuongeza mkataba wao wa udhamini. Akihojiwa na wanahabari Al Baker amesema kila kitu kinawezekana katika kampuni yao na hivi karibuni wanaweza kuongeza jina katika Uwanja wa Camp Nou. Makamu wa rais wa Barcelona Javier Faus alithibitisha kuwepo mazungumzo hayo na kudai kuwa wanaridhirishwa na mahusiano waliyonayo na kampuni hiyo kwnai hawatawahi kuwa na matatizo nao. Feus amesema kwasasa bado wanajadili lakini uamuzi wa mwisho utatolewa mwaka huu huu.

No comments:

Post a Comment