Thursday, February 5, 2015

MANCINI ACHUKIZWA INTER KUTOLEWA KOMBE LA ITALIA NA KUWAITA WACHEZAJI WAKE WAPUUZI.

MENEJA wa klabu ya Inter Milan, Roberto Mancini amegadhabishwa na wachezaji wake na kuwaita wapuuzi baada ya kukubali kufungwa bao katika dakika za mwisho jana katika mchezo wa Kombe la Italia dhidi ya Napoli. Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa San Paolo, Inter walionekana kama wataweza kuupeleka mchezo huo katika za nyongeza lakini makosa ya walinzi wake yalisababisha mchezo huo kumalizika katika muda wa kawaida. Zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya muda wa kawaida kumalizika Gonzalo Higuain aliwanyanyua mashabiki wa Napoli kwa kufunga bao pekee katika mchezo huo ambalo liliwavusha katika hatua ya nusu fainali huku Inter wao wakifungasha virago. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Mancini amesema hajui hata aseme nini kwani safu yake ya ulinzi imemuangusha kwa kukosa umakini katika muda muhimu. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa inauma kufungwa kama hivyo lakini upuuzi ulikuwa wa kwao kwa kulegea katika muda muhimu katika mchezo. Hicho kinakuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Inter wakati wakielekea katika mchezo wa Serie A Jumapili hii dhidi ya Palermo.

No comments:

Post a Comment