KLABU ya Celtic imetozwa faini ya paundi 7,300 na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kufuatia vurugu za mashabiki wake katika mchezo wa makundi ya Europa League dhidi ya Dinamo Zagreb. Hiyo inakuwa mara ya tano katika kipindi cha miaka mitatu Celtic kutozwa faini na UEFA kutokana na vurugu za mashabiki wao. Mashabiki hao walikwaana na polisi baada ya kurusha mafataki katika mchezo ambao Celtic walichapwa mabao 4-3 Desemba mwaka jana ingawa pamoja na kipigo hicho walifanikiwa kufuzu hatua ya timu 32 bora. Adhabu hiyo ya faini iliyotolewa na kamati ya maadili na nidhamu ya UEFA imekuja wakati Celtic na mashabiki wake wakisafiri kuelekea nchini Italia kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa pili wa michuano hiyo dhidi ya Inter Milan. Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Celtic walitoka sare ya kufungana mabao 3-3 na Inter katika mchezo uliofanyika jijinio Glasgow.
No comments:
Post a Comment