RAIS wa Shirikisho la Soka la Tunisia-FTF, Wadii Al Jarii amejiuzulu wadhifa wake katika kamati ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka huu. Tunisia walienguliwa katika michuano hiyo katika hatua ya robo fainali baada ya kutandikwa mabao 2-1 na wenyeji Guinea ya Ikweta huko Bata, Jumamosi iliyopita. Lakini Tunisia wameonyesha kuchanganywa na kipigo hicho akiwemo kocha Georges Leekens akimlaumu mwamuzi aliyechezesha mchezo huo kutoka Mauritius kupendelea wenyeji. Kwa wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya Tunisia, Al Jarii alijitoa katika kamati hiyo kufuatia nchi yake kuenguliwa katika michuano hiyo. Taarifa hizo ziliendelea kudai kuwa Chiheb Belkhiria ambaye ni mjumbe katika kamati ya fedha ya Shirikisho la Soka la Afrika-CAF naye aliachia wadhifa wake huo.
No comments:
Post a Comment