KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amesema michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2023 itasogezwa mbele kutoka Januari mpaka Juni ili kusaidia kusogezwa kwa michuano ya Kombe la Dunia 2022. Kikosi kazi cha FIFA kimependekeza Kombe la Dunia kuchezwa Novemba na Desemba ili kuepuka joto kali katika majira ya kiangazi nchini Qatar. Valcke amesema Shirikisho la Soka la Afrika-CAF limekubali kuwa halitafanya michuano hiyo ya Afcon Januari na badala yake watasogeza mbele mpaka Juni. Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 imepangwa kumalizika Desemba na michuano ya Mataifa ya Afrika yenyewe kwa kawaida ilitakiwa kuanza kuchezwa katikati ya mwezi Januari mwaka 2023.
No comments:
Post a Comment