MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Phil Neville amesema kuandaliwa kwa michuano ya Kombe la Dunia kati ya Novemba na Desemba mwaka 2022 nchini Qatar ni jambo zuri kuwahi kutokea kwa nchi yake. Kikosi kazi cha Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kilipendekeza michuano hiyo kuhamishwa wakati wa majira ya baridi kwasababu ya joto kali nchini Qatar. Wakati wadau wengi wakikosoa uamuzi huo, Neville yeye anafikiri michuano hiyo itakuwa na faida kubwa kwa matumaini ya Uingereza kunyakuwa taji hilo. Neville anaamini katika kipindi hicho wachezaji wanakuwa bado wako vyema na tayari kwa ajili ya kupambana na timu bora duniani. Mapendekezo hayo ambayo yanatarajiwa kufikishwa mbee ya kamati ya utendaji ya FIFA itakayokutana jijini Zurich, Machi mwaka huu, tayari inaungwa mkono na rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini, Shirikisho la Soka la Afrika-CAF, Concacaf na Shirikisho la Soka la Asia.
No comments:
Post a Comment