WAKILI wa mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius anayetumikia kifungo, wamefungua mashitaka kupinga waendesha mashitaka kukata rufani dhidi ya huku iliyotolewa kutokana na kosa lake la mauaji. Jaji Thokozile Masipa Desemba mwaka jana aliruhusu waendesha mashitaka kukata rufani kutokana na hukumu aliyotoa kama watahitaji kufanya hivyo. Masipa alimhukumu Pistorius kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua bila kukusudia baada ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari mwaka 2013. Pistorius alijitetea kuwa alimuua mpenzi wake huyo kimakosa akidhani kuwa ni jambazi, wakati waendesha mashitaka walikuwa wakidai kuwa alimuua kwa makusudi baada ya kutofautiana nyumbani kwake jijini Pretoria.
No comments:
Post a Comment